SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 28 Mei 2016

T media news

LEBRON AWEKA REKODI, CAVALIERS WATINGA FAINALI YA NBA.


Cleveland Cavaliers wamefanikiwa kutwaa ubingwa wao wa pili mfululizo kwa kanda ya Mashariki na sasa wanasubiri mshindi kati ya Golden State Warriors dhidi ya Oklahoma City Thunder ambao hata hivyo Thunder wanapewa nafasi kubwa kutokana na aina ya mchezo wanaoucheza sasa mpaka kufikia kuongoza 3-2.

Kwa LeBron James, hii ni mara ya sita mfuululizo kutinga Fainali ya NBA. Anakuwa mchezaji wa 8 kufanya hivyo katika historia ya NBA.

James alifunga pointi 33, Kevin Love alikuwa na pointi 20 na rebounds 12, na klabu ya Cavaliers ikatinga fainali yao ya pili mfululizo kwa kuichapa Toronto Raptors 113-87 katika mchezo wa sita wa fainali ya Mashariki iliyofanyika alfajiri ya Jumamosi.

Cavaliers itakuwa inataka kumaliza ukame wa miaka 52 wa kutokutwaa ubingwa wa NBA, ambao ni muda mrefu zaidi kwa mji wowote wenye timu angalau tatu za kimichezo. Hakuna timu inayotoka mji wa Cleveland ambayo imewahi kushinda taji lolote tangu Browns blanked Baltimore 27-0 kushinda NFL michuano ya mwaka 1964.

“Mji huu umekuwa na tamaa ya kutwaa ubingwa wa michuano hii,” alisema kocha Tyronn Lue. “Tuna timu nzuri na sahihi na tuna vipaji vizuri.”

James, ambaye alikulia katika mji jirani wa Akron, lazima anafahamu vyema ni kwa namna gani ubingwa wa michuano hii itakuwa na maana kubwa kwa mji wa Cleveland.

“Najua mji wetu unastahili kushinda ubingwa huu, mashabiki wetu wanastahili pia,” James alisema. “Lakini hiyo haitupi hisia ya kubweteka. Tumekuwa na bado tunatakiwa kutoka na kwenda kupambana. Bado tunatakiwa kutoka na kwenda kuchukua taji na kuthibitisha ubora wetu wenyewe.
Kyrie Irving alikuwa na pointi 30 na J.R. Smith aliongeza 15 kwa Cavaliers, ambayo inasubiri kukabiliana na mshindi wa fainali ya Magharibi kati ya Golden State-Oklahoma City ambayo imeingia mchezo wa sita na Thunder anaongoza 3-2.

Cleveland itaanza michezo yake nyumbani kama mabingwa wa Magharibi watakuwa Oklahoma City Thunder kutokana na rekodi zao za ushindi wa msimu huu lakini itaanza michezo yake ugenini kama itacheza dhidi ya Warriors waliokuwa na rekodi bora ya kushinda michezo 73.

Kyle Lowry alifunga pointi 35 na Demar DeRozan alikuwa na pointi 20. Raptors walishuhudia msimu wao bora kabisa katika historia ya klabu hiyo kwa kushinda michezo 56 huku pia wakishinda michezo yao ya mtoano mpaka fainali kwa mara ya kwanza. Mashabiki pia walihamasika na haikuwa ajabu kw atiketi zote 20,605 kuuzwa.

Katika kuonyesha wamefurahi kwa hatua ya timu yao ilipofikia muda wote walikuwa wakiimba kuiunga mkono hata katika dakika ambazo walionekana wasingeweza kurejea tena mchezoni.
Kocha wa Raptors Dwane Casey alisema kufikia mkutano fainali ilikuwa “ni hatua kubwa ya kujifunza na kuongeza uzoefu”

HIGHLIGHTS