DAR ES SALAAM
Waamuzi kutoka Afrika Kusini watachezesha mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Azam FC dhidi ya Esperance ya Tunisia.
Mechi hiyo itachezwa Aprili 10 kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi Dar es Salaam.
Azam inacheza hatua hiyo ya pili baada ya kuiondoa kwenye mashindano wawakilishi wa Afrika Kusini Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
Msemaji wa Azam Jaffer Idd alisema jana kuwa mechi ya marudiano itakayofanyika nchini Tunisia itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Hata hivyo, Idd hakuyataja majina ya waamuzi hao.Kuhusu kikosi chao, alisema kinaendelea na mazoezi chini ya Kocha Sterwart Hall.
“Tuna mechi za ligi na michezo miwili ya kimataifa. Tunafanya maandalizi kwa ajili ya mashindano yote hayo,” alisema Idd.
Aliongeza: “Wachezaji wote ikiondoa wale ambao wako na kikosi cha timu ya taifa wanaendele ana mazoezi.”