THIERY HENRY: SIKUFURAHIA KUCHEZA WINGA UFARANSA
Na Amin Amali
Mfungaji wa muda wote wa arsenal na pia mfungaji wa muda wote timu ya Taifa la France THIERY HENRY,
Ameliambia “The Sun” kuwa hakufurahishwa kuchezeshwa nafasi ya winga akiichezea timu ya taifa haswa 1998 wakati wanachukua kombe la dunia na miaka miwili baadae wanachukua ile ya mataifa ya ulaya
Henry mwenye miaka 38 ambapo alistaafu mpira mwaka 2014 kwa sasa anafundisha timu B ya arsenal.
“swala ni kwamba inatakiwa ufanye kazi kwa mipango ya timu na kulisaidia taifa lakini kucheza sehemu ambayo klabu yako huchezi hapo inatakiwa kujiandaa inatakiwa ukubali matakwa ya timu na yoyote ilie tayari kucheza na kulitetea taifa lake sikupendezwa kucheza winga lakini ilibidi” alimaliza hivyo Thiery Henry wakati ana hojiwa na The sun.
Moja ya matumaini ya shabiki wa Arsenal kumuona siku moja nyota huyo anaifundisha timu hiyo .