TAARIFA MPYA KUHUSU UJENZI WA BOMBA LA GESI
Na Martha Magawa
Wizara ya Nishati na Madini Inaendesha mkutano na wafanyabiashara wa mafuta nchini ambao utalenga kuibua fursa zitakazo jitokeza katika mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta litakalo jengwa kuanzia HOIMA
nchini Uganda hadi bandari ya Jijini Tanga.
Akizungumza na wanahabari Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa amebainisha fursa zitakazojitokeza kupitia mradi huo kuwa ni pamoja na kupata tenda, ajira kwa vijana, kodi
itakusanywa kupitia mradi huo wa ujenzi.
“Mradi huo utapitia nchini lakini pia utaibua fursa mbalimbali zikiwemo ajira,tenda na utaongeza pato la Taifa kupitia ukusanyaji wa kodi”. Alisema
Katibu
Aidha Ntalikwa ameongeza kuwa ujenzi huo utaendeshwa kwa miezi thelathini na sita (36) na utaanza mara tu baada ya makubaliano baina ya Tanzania, Kenya na Uganda ambapo dalili zinaonesha wazi kuwa bomba litajengwa Tanzania kulingana na sifa ya nchi hiyo kuwa na Vigezo husika kama Uzoefu,Amani na Ulinzi.