Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paulo Makonda amemwagiza Ofisa Elimu,Raymond Mapunda kuitisha mkutano wa walimu March 26 mwaka huu ili kujadili matarizo yanayowakabili likiwemo la kutopanda madaraja kwa wakati.
Makonda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akikabidhi madawati 500 katika shule ya msingi Kawawa yaliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Mkuu huyo alieleza kuwa yapo matatizo mengi yanayowakabili walimu yanayotokana na watu wanaojinufaisha matumbo yao kwa kuwalipa walimu hewa
Katika hatua nyingine,Makonda aliwataka walimu kutovunjwa moyo kutokana na matatizo yaliyopo katika sekta ya Elimu.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,Diego Gutierrez alisema kuwa mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni ya Tigo kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo ya elimu nchini