Huyo ndio Adi Yussuf anaecheza ligi daraja la pili nchini uingereza. amezaliwa Zanzibar tarehe 03/10/1992 anavaa jezi na 18 akicheza nafasi ya straiker. alianza mpira katika club ya Leicester City lakini hakuweza kucheza hata mech moja akiwa katika team hiyo ya watoto, mwaka 2011 baada ya mkataba kuisha aliondoka na kujiunga na Tamworth kwa mkopo. alicheza mechi kumi (10) na kufunga magoli mawili (2).
2011-2013 alijiunga na Burton Albion, aliweza kucheza mechi ishirini na tano (25) na kufunga goli moja (1).
2013-2014. Adi aliweza kucheza katiba timu nyingine ambazo ni Lincoln City, Gainsborough trinity (loan), Harrogate Town (loan) na Histon (loan).
2014 - 2015 Adi alinunuliwa na timu ya Oxford city na kuweza kucheza mechi thelathini na tisa (39) huku akiipatia timu yake magoli ishirini na saba (27). na hapo ndipo nyota ya Adi alianza kuonekana.
2015 - 2016 Adi alinunuliwa na timu ya Mansfield inayoshiriki ligi daraja la pili maarufu kama League Two, na kufanikiwa kucheza idadi ya mechi ishirini na moja (21) hadi hivi sasa huku akiwa na magoli matano (5). akiwa katika timu hii ameweza kucheza mech za FA cup mbili (2).
Pongezi za dhati zimuendee kocha wa timu ya taifa Charles Boniphace Mkwasa kwa kuweza kuwaonesha watanzania kua kuna wachezaji wa hapa kwetu wapo ulaya ila tu hawapewi nafasi ya kuisaidia timu yetu ya taifa.