NimekomaAliyetamka neno hilo ni mwanadada anayefanya poa kwenye muziki, Linah ambapo amesema kuwa, amekoma kuwaanika wapenzi wake kwani amegundua ndiyo sababu ya kutodumu nao.
Linah alimtonya paparazi wetu kuwa, amekuwa akijiuliza sababu ya kutodumu na wapenzi wake akagundua ile tabia ya kujiposti kimahaba na wapenzi wake ndiyo chanzo.
“Huwa sipendi kuwa na mtu kisha nikaachana naye, hasa yule ambaye moyo wangu umemkubali, lakini ilikuwa kila ninayeingia naye kwenye uhusiano, nikishaanza tu kumuanika huanza kujitokeza mambo ya kutuachanisha.
“Wengine ndipo wanapopata nafasi ya kuniharibia kwa kumpelekea vijineno na mwishowe tunaachana,” alisema Linah ambaye mara ya mwisho alikuwa akitoka na jamaa aitwaye William Bugeme.