Lakini kwa nini suala la Nyuklia lichangie vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran?
Ipo hivi, Iran hairuhusiwi kuwa na silaha ya nyuklia hasa kutokana na sheria za kimataifa, usalama wa dunia na siasa za kimataifa.
Iran ilitia saini mkataba wa kimataifa wa Nyuklia - Treaty on the Non-Proliferation of Nuclear Weapons (NPT) mwaka 1968.
Kwa kusaini mkataba huu, Iran ilikubali, kutotengeza silaha za nyuklia, kuruhusu ukaguzi wa nyuklia na International Atomic Energy Agency (IAEA).
Kwa hiyo kisheria Iran inaruhusiwa kutumia nyuklia kwa umeme, tiba, na utafiti, lakini si kwa kutengeneza bomu la nyuklia.
Lakini pia lipo suala la hofu ya usalama wa dunia. Nchi nyingi zinaogopa kuwa ikiwa Iran itapatra bomu la nyuklia, itasababisha mbio za silaha za nyuklia katikka Mashariki ya Kati. Kwamba nchi kama Saudi Arabia, Uturuki, au Misri zinaweza pia kutaka mabomu yao. Hii inaweza kufanya eneo hilo lenye migogoro kuwa hatari zaidi duniani.Vilevile yapo makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.
Hapa kulikuwa na makubaliano makubwa yanayoitwa Joint Comprehensive Plan of Action (JCPOA) ambapo, Iran ilikubali kupunguza shughuli za nyuklia. Kutokana na makubaliano hayo nchi za Magharibi zikaondoa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi, lengo hapa lilikuwa kuhakikisha Iran haitengenezi silaha ya nyuklia.
Kwa kifupi kutokana na maafikiano hayo, Iran hairuhusiwi kuwa na silaha ya nyuklia kwa sababu ilisaini mikataba ya kimataifa ya kutokuzalisha mabomu hayo, na pia dunia inaogopa kuwa bomu la Iran linaweza kusababisha hatari kubwa ya vita au mashindano ya silaha.
Hata hivyo mataifa kama vile Marekani, Urusi,Uingereza, Ufaransa na Uchina yalitambuliwa chini ya mkataba wa
Treaty on the Non-Proliferation of Nuclear Weapons (NPT), kuwa na silaha hizo. Ipo hivi mataifahaya ambayo mara nyingi huitwa “Nuclear Weapon States” yalikuwa na silaha hizo kabla ya mwaka 1967.
