Kiongozi mkuu wa usalama wa taifa wa Iran Ali Larijani amesema wanajeshi kadhaa wa Marekani wamekamatwa wakati wa mzozo wa hivi karibuni kati ya Marekani, Israel na Iran.
Larijani, ambaye ni katibu wa baraza kuu la usalama la Iran alisema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X siku ya Jumapili:
“Nimepata taarifa kuwa wanajeshi kadhaa wa Marekani wamechukuliwa mateka. Lakini Wamarekani wanadai kuwa wameuawa vitani. Licha ya juhudi zao za kuficha ukweli, ukweli huo hauwezi kufichwa kwa muda mrefu.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tangu mwishoni mwa mwezi uliopita Marekani na Israel zimeanza mashambulizi mapya dhidi ya Iran, jambo ambalo limesababisha Iran kujibu kwa mashambulizi makubwa.
Jeshi la Iran, hasa Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC), linasemekana kurusha mamia ya makombora ya ballistic na ndege zisizo na rubani (drones) dhidi ya malengo muhimu ya kijeshi ya maadui wao.
Siku moja kabla ya kauli hii, Larijani alikuwa tayari ameonya kwamba hatua za Washington zitakabiliwa na majibu makali kutoka Iran.
Chanzo Irannews
