SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 20 Aprili 2018

T media news

Muvi 5 bora zaidi kuzitazama kabla hujafikisha miaka 30 (na baada ya miaka 18)

Wengi wanakiita kipindi cha ujana. 20s. Hapa unakuwa umemaliza ule ujana wa mwanzo mwanzo, 18 na 19, ndo umeingia kwenye 20 lakini bado hujafika 30. Tanzania watu wenye umri huu baadhi wanakuwa chuo, au wamemaliza au wako tayari mitaani wanapambana na maisha kujipatia riziki zao. Wengine umri huu wanakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, baadhi ndo unakuta wameanza, wengine unakuta wana uzoefu, wengine unakuta hata wameshaoa au kuolewa na kuwa na familia.

Wengine huu ni muda wa stress za hali ya juu, wakati mwingine unaona maisha hayaendi, malengo yako hayatimii, unajiuliza mara kibao nini maana ya maisha. Wengine unakuta mapenzi yamekuwa machungu na wanaapa kutoacha moyo ujiongoze tena.

Haijalisha uko katika hali gani lakini hapa chini tumekuwekea muvi 10 ambazo zinaweza kusukuma siku yako na kukupa mitazamo tofauti ya maisha. Muvi sio mpya ila ni timeless, maudhui yake yanadumu.

 

“The Graduate”

Hii movie ni ya mwaka 1967. Muvi ni ya maisha ya jamaa ambaye amemaliza elimu yake chuoni lakini hana kazi, kajawa na stress na kibaya zaidi kaingia katika mahusiano na mama ya mpenzi wake. Muvi nzuri na inakupa picha ya jinsi maamuzi yetu yatakavyoathiri maisha yetu, hata maamuzi ambayo unaweza kuona haya ya kawaida sana.

 

“Groundhog Day”

Hii muvi inaonyesha namna gani ambavyo kuna siku unafika unachoka na kile ambacho unakifanya, inaonyesha namna gani maisha yanakuwa hayana maana kama kila siku utafanya kitu kile kile tu na kwa nini lazima ufanye mambo mbalimbali ili maisha yaweze kuwa maana.

“Touki Bouki”

 

Hii muvi imechezwa Senegal. Inaonyesha mtu na mpenzi wake ambao walitamani sana kwenda Paris Ufaransa kutalii lakini hawana hela. Inaonyesha namna ambavyo walipambana kupata hela ya kwenda na vikwazo ambavyo walipitia. Mtu yeyote mwenye ndoto ya kufanya kitu kikubwa kwenye maisha ataipenda hii muvi.

 

 

“Red Beard”

Ushawahi kusikia stori za mshikaji wako kupangiwa kazi kwenye mazingira magumu kijiji hata hakina barabara? Au ushasikia mshikaji wako kaenda kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo kutafuta mawe? Au mtu yeyote aliyeamua kuondoka sehemu moja na kwenda sehemu ambayo haijui kabisa kuanza maisha? (Stori za wazee wa zamani Dar wanakwambia kuna baadhi walikuja na mbio za Mwenge na walikuwa hawamjui mtu Dar). Kama hivyo. Hii muvi ni stori ya Daktari kijana ambaye alitoka mjini akapangiwa kazi kijijini. Muvi ni stori ya namna ambavyo alijipanga na kuishi maisha katika eneo ambalo hakuwa kujua atakuja kwenda.

 

“The Social Network”

 

Unakataliwa na msichana au mvulana ambaye unampenda kisa tu hauna swaga au huna hela. Unaamua kutafuta hiyo swaga na hela kwa namna yoyote, unapitia vikwazo, unaanguka, unasimama mpaka unatoboa na kuishangaza dunia. Hii ni muvi ya aina hiyo.