SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 11 Aprili 2018

T media news

Makosa makubwa mawili unayoyafanya kila mara unapotumia choo

Choo ni kitu muhimu sana katika nyumba. Wengine huenda mbali zaidi na kusema kwamba nyumba ni choo, wakimaanisha kuwa, ili nyumba yako ionekane bora, basi lazima uwe na choo kilicho bora.

Watu wengi wanapokwenda chooni hufanya makosa mbalimbali ama kwa kujua au kwa kutokujua ambapo baadhi ya makossa hayo husababisha matatizo ya kiafya kwa watu wengine.

Tuangalie kwa ufupi baadhi ya mambo mawili ambayo tumekuwa tukikosea kila mara tunapotumia vyoo kujisaidia au kwa shughuli nyingine.

Watu wengi sana, hasa wanaotumia vyoo vya kuketi, hufungulia maji (flush) wakiwa hawajafunika choo baada ya kujisaidia. Usahihi ni kuwa, kabla ya kusukuma kinyesi kwa maji, unapaswa kufunika kwanza choo chako na mfuniko uliopo, na kisha ufungue maji.

Unapofungulia maji angali bado haujafunika choo chako, baadhi ya chembechembe kutoka ndani ya choo zinaweza kuruka na kutoka ndani ya choo hadi umbali wa futi 6, kutokana na nguvu (pressure) ya maji.

Kitendo hicho kinaweza kusababisha maradhi kwa watu mbalimbali kutokana na uchafu uliotoka ndani ya choo. Kuepuka hilo, hakikisha kila unapotumia choo, unafunika kwanza kabla ya kufungua maji ili kuondoa kinyesi.

Jambo linguine ni kuwa, watu wengi hupendelea kuweka miswaki yao chooni lakini kosa kubwa wanalolifanya ni huweka miswaki hiyo ndani ya vikopo kwa kile wanachoamini kuwa kwa kufanya hivyo wanazuia bakteria kufikia miswaki.

Unapoweka mswaki ndani ya kopo, unaufanya mswaki huo upate shida kukauka vizuri mara baada ya kutumiwa na unaweza kutengeneza mazingira ya baketria kuishi.

Unachoshauriwa kufanya ni kuweka mswaki wako katika eneo la wazi huku sehemu ya kuswakia ikiwa imekaa juu ili kuupa nafasi ya kukauka vizuri. Pia, hakikisha mswaki huo haugusani na mswaki mwingine katika sehemu ya kuswakia.