MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU, "MWENYEWE AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAKANISA, MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE SANAMU YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO SI KWELI
Ikiwa leo ni siku ya JUMANNE tulivuu T MEDIA NEWS imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel,
T MEDIA NEWS7 imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo YESU au ISSA BIN MARYAM kama wanavyomuita Waislamu .
hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
BRIAN DEACON NDANI YA FILAMU YA ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,
ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
#Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.
Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga,
,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.
ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
BRIAN ANAWAAMBIA WATU WOTE DUNIANI KUWA YEYE SI YESU BALI YEYE NI MUIGIZAJI TU, WALA HAFANANI NA YESU KWANI ENZI ZA YESU HAPAKUWEPO NA TEKNOLOGIA YA CAMERA HIVYO HATA SURA HALISI YA YESU HAIJULIKANI ZAIDI YA WATU KUOTEA NA KUBUNI JINSI YESU ALIVYOFANANA KAMA DIRECTOR WAKE ALIVYOBUNI KWA DEACON
BRIAN PIA AMESHANGAZWA NA BAADHI YA WAUMINI KUWEKA PICHA ZAKE KWENYE MAJUMBA YAO NA KUVAA ROSARI ZENYE PICHA YAKE WAKIAMINI YEYE NI YESU KITU AMBACHO NI MAKOSA
AMESEMA ILI KUTHIBITISHA KUWA YEYE NI MUIGIZAJI TU AMEZITAJA filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. (sadickTV © NIMEIANDAA KWA MSAADA WA MTANDAO , DEACON PROJECT , TRUTH MUST BE FOUND