SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 5 Aprili 2018

T media news

Vitu vitano vya kufanya kila siku asubuhi uwe na siku njema

Ratiba za Watanzania wengi asubuhi hufanana ambapo wengi huamka, kisha kifungua kinywa na majukumu mengine huendelea. Lakini ni wachache wanaojua kuwa kuna vitu vichache unaweza kuviongeza hapo na ukaanza asubuhi vizuri na siku yako ikaisha kwa kuwa na ari katika utendaji kazi wako.

Hapa chini tutaeleza mambo matano muhimu ambayo ni vyema ukayafanya kila asubuhi. Vitu hivyo sio vigeni, wengi wanavifahamu, lakini ni vile huamua kutokuvifanya kutokana na sababu mbalimbali.

1. Sugua kwa utaratibu (massage) masikio yako

Kusugua masikio yako kwa utaraibu (massage) kutakuwezesha wewe kuamka vizuri. Unatakiwa kufanya hivyo ukiwa bado umelala kitandani. Kusisimua meneo yenye hisia ya sikio lako itakufanya kuwa na matokeo chanya kwako na kukufanya ujisikie vizuri siku nzima.

 

2. Kunywa maji ya uvuguvugu yenye limao

Kuna sababu nyingi sana kwanini ni vyema kuacha kunywa kahawa asubuhi na badala yake unywe maji yenye uvuguvugu. Hii itakusaidia kuimarisha mfumo wako wa mmengenyo wa chakula, figo, na utumbo, itaondoa sumu mwilini, kuongeza kinga ya mwili na faida nyingine ambazo ni za wazi kuonekana.

Huhitaji kutumia limao zima bali hata robo tu ya limao inatosha kuchanganya kwenye glasi moja ya maji. Kama ukiamua kunywa maji haya, unashauriwa kukaa hadi dakika 30 kabla ya kunywa chai au chakula kingine.

3. Safisha ulimi wako

Wote tunafahamu kwamba unatakiwa kusafisha kinywa chako mara mbili kwa siku. Lakini haupaswi kuishia hapo kwa sababu aina nyingi sana ya bakteria hukusanyika katika ulimi wako, na hiyo huweza kupelekea wewe kutoa harufu mbaya mdomoni, kuharibika kwa meno, au kupata tatizo katika taya zako.

Ili kusafisha ulimi wako, unahitaji kuwa na mswaki wa kawaida. Kuwa mwangalifu unaposafisha usitumie nguvu sana ili kutokuathiri ulimi wako.

4. Kula kijiko kimoja cha asali

Asali inakusaidia kupata nguvu, kuwa na kumbukumbu nzuri, mwili ulioimara, inatibu kikohozi, na pia husaidia katika tatizo la aleji. Kutokana na sababu hizi na nyingine nyingi, unashauriwa kuanza siku kwa kunywa kijiko kimoja cha asali.

Iwe ni asali nzuri na ya asili na unatakiwa kunywa dakika 10 hadi 15 kabla ya kupata kifungua kinywa. Kama kwako unaona ni tamu sana, unaweza kuchanganya kwenye maji kwani faida zake zitabaki palepale.

5. Safisha kinywa chako na hydrogen peroxide solution

Jambo la tano unaloshauriwa kulifanya asubuhi ni kusafisha kinywa chako kwa kutumia hydrogen peroxide solution. Hakuna madhara yatokanayo na kuitumia kama utatumia katika kiwango kinachoshauriwa ambacho ni matone 5-7 ya 3% kwa maji 50ml. Pia, kumbuka kuweka mchanganyiko wako kwenye maji kuliko kufanya vinginevyo.

Hatua hii itakusadia kungarisha meno yako, kukuepusha na harufu mbaya mdomoni na pia kulinda na kutunza taya zako.