SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Machi 2018

T media news

Dada Jifunze Alafu Badilika Namna Unavyojiweka



Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasua? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.