SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 15 Februari 2018

T media news

Marekani Yalaani Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA, Daniel John na Majeraha Aliyopatiwa Reginald Mallya.

Marekani imesikitishwa sana na taarifa za kutekwa na utumiaji nguvu kikatili uliosababisha kifo cha Daniel John na majeraha kwa Reginald Mallya.

Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu. Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana. Tunatoa wito kwa vyama vyote kulinda amani na usalama wa mchakato wa kidemokrasia, taifa na wa watu wa Tanzania.

Aidha, tunaungana na Watanzania katika kutoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania