Hii ni baada ya Waziri Mkuu KASIMU MAJALIWA kufanya Mkutano wa hadhara mjini Bunda katika Uwanja wa Sabasaba na kuwaeleza wananchi Kwamba serikali ilitoa shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya mradi wa maji lakini umeshindwa kukamilika kwa wakati huku mamlaka hiyo kupitia kwa Fundi bomba mkuu wake bwana Mansour Mandemla akisema kwamba wameshafanikisha mradi kwa asilimia 98 jambo ambalo waziri mkuu hakukubaliana nalo.
Aidha amewaagiza Mkandarasi wa mradi huo,meneja wa maji Bunda }Buwasa},Meneja wa majiMusoma }MUWASA}, Wabunge wa majimbo za wilaya ya Bunda na Mkuu wa wilaya Mwl, Lydia Bupilipili wakutane ikulu kujadili suala hilo la maji kwa kina kabla hajachukua mamuzi.
Kwenye picha hapo ni Waziri Mkuu akikagua mashine za kusukuma maji yaliyoko kata ya Bunda stoo wakati wa ziara yake wilayani hapa.wakati kabla ajazungumza na wakazi wa bunda
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amewakabidhi hati ya usajili wa chama viongozi wa chama cha ushirika cha Igembe sabo cha Bunda,Malongo Mashimo ambae ni katibu na Maria Nengwa ambae ni mwenyekiti wa ujenzi,
Waziri Mkuu amekabidhi hati hiyo baada ya Kufanya uzinduzi wa Ushirika huo akiwa katika ziara wilayani Bunda leo january 19.2018.

