Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa jinsi utawala wa awamu ya tano unavyoongoza nchi, inahitaji ujasiri wa ziada kusimama na kuusifia.
Mbowe amesema hay oleo Jumanne muda mchache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenda Ikulu.
Amesema mwaliko wa Lowassa ni wake binafsi na wala hauhusiani na Chadema na hata kile alichokizungumza cha kumsifia Rais Magufuli ni mawazo yake binafsi.