SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 10 Januari 2018

T media news

Makonda, Ally Hapi Wamuandikia Ujumbe Huu Mbowe

January 9 2018 kuna mambo mengi yametokea na yame-trend katika mitandao ya kijamii kutokana na uzito wake, ikiwa ni pamoja na  Rais John Pombe Magufuli kukutana na waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.

RC Makonda amepost picha ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe na kuandika “Kaka yangu mpendwa anawatakia usiku mwema”>>>RC Makonda

Post ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliyoipost usiku wa January 9 katika ukurasa wake wa instagram imeonekana ku-trend kwa kupata likes nyingi na comment katika kipindi cha muda mfupi


Naye  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi aliposti picha ya Mbowe na Kuandika maneno ambayo ni mafumbo kwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani aliandika "kwa hisani ya joto la Dar es Salaam"