Benki Kuu ya Tanzania ni taasisi ya umma ambayo ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 14 Juni 1966 kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu Na. 12 ya mwaka 1965. Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1978. Aidha, mwaka 1995 ilitungwa sheria mpya ya Benki Kuu na kufanyiwa maboresho mwaka 2006 ili kutoa mamlaka zaidi kwa Benki Kuu katika kusimamia utekelezaji wa sera ya fedha.
Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.
Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania yapo Mtaa wa 2 Mirambo; 11884 Dar es Salaam. Benki Kuu pia ina matawi Zanzibar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Mtwara na Chuo cha Benki Kuu kilichopo jijini Mwanza.
Tangu Benki Kuu ilipoanza kufanya kazi mwaka 1966 hadi sasa, imekuwa na jumla ya magavana 7 na naibu magavana 11 ambao wameongoza benki hiyo kwa vipindi tofauti.
Hapa chin ni orodha ya magavana walioiongoza Benki Kuu ya Tanzania hadi sasa;
7. Prof Florens Luoga (3/Jan/2018- Hadi sasa)
6. Prof. Benno Ndulu (8/Jan/2008- 3/Jan/2018)
5. Dkt. Daudi T.S. Ballali (1998 hadi 8/Januari/2008)
4. Dkt. Idris. M. Rashidi (1993 hadi 1998)
3. Bw. Gilman Rutihinda (1989 hadi 1993)
2. Bw. Charles Nyirabu (1974 hadi 1989)
1. Bw. Edwin I. Mtei (1966 hadi 1974)