‘Eti kwasababu takataka zinatupwa jalalani haimaanishi kuwa takataka ni uchafu’
Kulingana na ripoti ya world bank , Afrika inazalisha zaidi ya tani millioni 70 kwa mwaka. Kwa wastani, waafrika tunazalisha zaidi ya kilogramu moja kila siku kila mtu. Kila mwaka kiwango cha takataka kinachozalishwa kinaongezeka. Sababu ya kuongezeka kwa takataka ni kutokana na idadi ya watu wanaoongezeka. Kila mtu hapa ni kiwanda kidogo kinachozalisha takataka.
{Mkurugenzi wa Zaidi Enterprises Mr. Allen Kimambo anayetengeneza mamilioni kupitia takataka}Takataka ni nini? Ni kitu chochote kilicho poteza thamani ya kutumika na kutupwa.
Takataka hizo zinaweza kuwa paper bags, makaratasi, makopo, maboksi yaliyotupwa, mabaki ya vyakula, mabaki ya jikoni, kinyesi, nguo zilizoisha nk. Jambo la kushangaza takataka kwa mtu wa kawaida ni uchafu wakati kwa nchi zilizoendelea takataka ni biashara ya mabilioni ya pesa.
Nchi kama Amerika ya kusini na ulaya kuna viwanda vya mamilioni kwasababu ya takataka. Takataka ni madini. Afrika, sekta ya takataka bado sana. Ingawa wapo wajasiriamali wachache, wajanja wanaotumia takataka kujitajirisha. Tutagusia fursa zitokanazo na takataka na kuwachambua watu waliofanikiwa kwa kutumia takataka.
Fursa katika takataka ni pamoja na Kutoa huduma ya kukusanya na kuziweka takataka sehemu sahihi. Kuna watu wanahangaika wapi wakatupe takataka hasa mijini. Ninawajua watu waliojitajirisha Tanzania kwa kuzoa takataka tu.
Yupo kijana mmoja jina lake ni Mohamed Mwale ameweza kujipatia pesa kutoka kwa wawekezaji kwa msaada wa mfuko wa Rais kwa kuzoa takataka.
Mr. Allen Kimambo mkurugenzi wa Zaidi Enterprises hivi karibuni ameingia kwenye 50 bora katika mashindano ya biashara bora inayogusa jamii Afrika. Ni kupitia takataka.
Wakati wengine tunaleta usharobaro kuna wengine wapo mtaani wanakusanya mamilioni ya pesa kwa kuzoa takataka. Fikiria kinyesi- maeneo ya mijini hakuna vyoo vya kutosha kabisa. Mfano Dar es salaam ni kampuni chache sana zinazokusanya takataka. Kuna uhitaji sana hapa.
Katika kukusanya takataka hasa kinyesi- unaweza kuanzisha mobile toilets company. Ni rahisi sana. Yapo makampuni ya kuhesabu yanayotoa huduma hii kwa mobile toilets. Yupo mtu mmoja karibu masaki ana mobile toilets nyingi. Anaingiza pesa sana. Ili uingie vizuri hapa watafute watu waliofanikiwa katika mobile toilets, tafuta njia ya kuwatafutia masoko. Wakikuamini jikite kwa kusoma mfumo- who knows unaweza kuwa partner pia. Kumbuka wafadhili pamoja na Development organizations wanatafuta mtu kama wewe utakayefanya biashara ya kutunza mazingira. Unaweza kuitwa TEDX kwasababu ya biashara hii.
Pia takataka kama kinyesi- kuna tekinolojia ya wahindi na Brazil unaweza kutumia kutengeneza chanzo cha nguvu-umeme etc. Maeneo ya vijijini ukisoma vizuri na kutumia tekinolojia walahi utakuwa kama mesiah kwao.
Unamjua Isaac Durojaiye- mwanzilishi wa DMT Mobile toilets?
Ukiingia kwenye hii biashara utakutana na DMT mobile toilets. Huyu jamaa alianzisha Diginified Mobile toilets baada ya siku moja akiwa kwenye mkutano akabanwa haja na kuingia msituni. Ana kiwanda sasa.
Isaac alianza biashara ya mobile toilets kwa kujenga kibanda mwenyewe. Siyo lazima uanze kujenga unaweza kutumia mfumo wake. Hivi karibuni Isack ametajwa na Forbes, pia CNN kutokana na mafanikio yake. DMT utakutana nazo kwenye majengo mikutano mpaka ya Mwakasege, maeneo ya ujenzi, kwenye matamasha makubwa mpaka fiesta. Fursa itakayofuata katika takataka ni Recycling. Kubadilisha takataka kuwa bidhaa nyingine. Najua itakushangaza.
Tutaendelea kuchambua kiundani kuhusu fursa hii…endelea kutufuatilia.
Ingia katika website yetu hapa: Nunua bidhaa za watanzania wenzako walioamua kuwa chanzo cha mapinduzi Tanzania na Afrika.