“Hatupo katika kizazi cha taarifa na maarifa. Tupo katika kizazi cha BURUDANI na STAREHE .” Tony Robbins
Burudani ni biashara inayokua kwa kasi sana AFRIKA zaidi ya kawaida. Sekta ya burudani imejaa fursa nyingi sana kupita kawaida.
Kila siku mamilioni ya watu duniani wanahangaika kutafuta sehemu za kustarehe, vitu vya kujistarehesha na kujiburudisha, michezo na matamasha ya kufurahisha.
Burudani ni sekta inayokua kwa kasi sana Afrika zaidi ya kawaida. Yeyote atakayeamua kuichunguza sekta hii kwa makini atashangaa fursa zilizojaa.
Sekta ya burudani inatengeneza zaidi ya $50 billioni kila mwaka. Sekta hii inaongoza katika kutengeneza ajira kuliko sekta zote Afrika.
Afrika ikiwa kama sehemu ya kivutio cha utalii, vipaji vya filamu na muziki bado vibichi. Dunia nzima inahamia Afrika kwasababu Afrika inaendelea kukua na kukua katika sekta ya burudani.
Tunaanza kuchambua Fursa sasa…
FURSA YA FILAMU NA MUZIKI.
Filamu na muziki hii hapa!!!!!! Sijui nianzie wapi katika Fursa hii. Sekta ya Filamu na muziki inakuja kwa kasi zaidi ya kawaida. Imejaa vipaji visivyo na kikomo. Hii fursa bado mbichi sana Tanzania. Angekuwa mwanamke ningesema hii fursa ni bikra. Bado haijaguswa vya kutosha. Kila siku makampuni ya filamu, sanaa na habari yanasajiliwa.
Mwaka 2015 GDP yake imekua kwa 5%. Ukichunguza waigizaji, waimbaji kama akina Diamond Platnum wanaingiza pesa nyingi kwa mwezi kuliko wakurugenzi wakubwa Afrika. Wasanii katika burudani hawa watu ni zaidi ya kawaida. Watu hawa wapo juu ya kilele. Msanii katika burudani anaweza kuingiza pesa nyingi ndani ya dakika tano pesa ambayo mtu mwingine anaweza kuipata kama akikusanya pesa hizo tokea utotoni mpaka uzeeni. Wao wanaweza kutengeneza ndani ya dakika tano. Hebu fikiria ni sawa kweli? Tuendelee….serikali inaweza kujipatia kodi kubwa hapa ikiangalia kwa jicho lingine
Hata ukiwa fisadi serikalini huwezi kushindana nao. Sekta hii Imejaa pesa nje nje kuliko kawaida. Laiti kama Merehemu Kanumba angekuwepo tungekuwa tunaongea lugha nyingine katika upande wa filamu. Nimekutana na waigizaji wengi maarufu …nasikitika kusema kuwa bado hawajagusa kabisa sekta hii. Kuna kauzembe fulani ka kufikiri hapa na wanajua. Hakuna focus hapa. Kuna ubabaishaji uliopindukia. Hii ndiyo sababu tunawasikia wanatumika na wanasiasa. Msanii wa filamu ni mtu mkubwa sana duniani..siyo mtu wa mchezo mchezo lakini wasanii wetu Mungu awasaidie..manake hawajaamka. Fursa 101 inataka kuwaamsha
Wako wapi wafanyabiashara wajanja afrika waweze kuichangamkia Fursa ya filamu Tanzania? Watanzania wanatamani kuona filamu zilizobamba lakini hazipo sokoni. Hakuna filamu nzuri sasa. Wasanii waseme wenyewe…mauzo ya filamu za kibongo yakoje kwasasa? Yameshuka kuliko kawaida. Hii haimaanishi watanzania hawapendi filamu, ila ni kwamba hamna filamu za maana.
Hii ndiyo sababu series za Udaan Sapnon Ki| maarufu kama Charkoli imebamba… tena imetafsiriwa hovyohovyo. Hebu fikiria kama badala ya umaarufu wa Udaan Sapnon Ki, tufanye ingekuwa ni filamu mpya ya wema sepetu ni kiasi gani cha kodi serikali ingekusanya? Lakini hao wanaotafsiri hizo filamu ..wanalipa kodi? Mnajua wanaharibu kwa kiasi gani sekta ya filamu Tanzania? Nisingependa kuwasema wao, sababu kubwa kwanini wametamba na kupata umaarufu ni wasanii katika filamu. Wamelala …wamesahau kuwa sanaa ndiyo inayoweza kutengeneza pesa nyingi sana kuliko hata kazi za kuvaa tai posta.
Tukianza na Nollywood, huko Nigeria. Unapoongelea Nollywood wamegusa kiasi kidogo sana katika sekta hii ya filamu Afrika. Yaani bado. Nollywood tu peke yake ina thamani ya $800 millioni. Katika nchi kama Nigeria yenye matatizo ya ukosefu wa ajira, Nollywood peke yake inaajiri zaidi ya mamilioni ya watu na kuifanya sekta hii ya filamu kuongoza baada ya sekta ya kilimo. Utafiti unaonyesha kuwa sekta hii ikiwekewa nguvu inaweza kuajiri watu wengi sana hata wale wasio na elimu.
Swali ni kwamba tupo serious au tumendeikeza ubabaishaji mwingi? Akina Wema Sepetu..na wengine vipi? Nini kimetusibu jamani? Tunakimbilia kwenye siasa..? Siasa? Wapo wasomi wengi mitaani wamefungwa na vyeti vyao wana vipaji lukuki na wana uwezo wa kuanzisha makampuni ya filamu Tanzania lakini wamelala fofo. Usingizi mzito.. Sijui wataamka lini…FURSA 101 imekuja kutufumbua macho
Nimekutana na vijana wa kawaida sana hawajaenda hata shule, hawajui hata kuandika lakini katika filamu…wamejiajiri na wanaingiza pesa kijinga jinga kuliko hata mameneja. Wanamiliki makampuni tena mengine hayajasajiliwa. Hebu fikiria
Waafrika wengi wanapenda starehe. Narudia tena…waafrika wengi tunapenda kuburudishwa. Hii ni fursa. Tangu Nollywood ianzishwe imekua kwa kasi sana sana…. na kuchukua nafasi ya pili duniani baada ya Bollywood katika idadi ya filamu zinazotengenezwa kila siku. Nollywood peke yake inatengeneza filamu 2000 kila mwaka baada ya Bollywood kutoka india inayotengeneza filamu 3000 kwa mwaka. Ikifuatia na Hollywood , Marekani inayotengeneza filamu 800 kwa mwaka.
Fursa katika filamu na muziki ni zaidi ya kawaida hapa Afrika hasa Tanzania. Waulize akina Joseph Kussaga mmiliki wa Clouds Media Group utashangaa pesa anazoingiza…mpaka kufungua makampuni mengine zaidi Dubai. Waulize Steps Entertainment na wengine wengi utashangaa. Waliwezaje? Ninampongeza san asana DJ Majey mmiliki wa Efm kwa kasi yake upande wa burudani. Nina hakika wapo wengi sana wanaweza kufanya zaidi ya hawa.
Idadi ya watu Afrika inakua kwa kasi sana. Matatizo ya usambazaji wa kazi za sanaa, muziki na filamu inaifanya Afrika kuwa mbichi sana katika sekta hii. Sasa kwa watu wenye mawazo hasi wataishia kuongelea matatizo yaliyopo ndani ya sekta. Sijui piracy..sijui kazi za sanaa zinaporwa. Nikuambie ukweli yeyote atakayeingia na kutatua matatizo yaliyo ndani ya sekta hii ni billionea wa Afrika. Waulize wasanii wengi maarufu Tanzania wana filamu ngapi zilizochezwa lakini wameziweka kapuni kwasababu hajatokea mjasiriamali mjanja Afrika anayeweza kutatua matatizo yaliyo ndani ya Sekta hii upande wa usambazaji. Lakini pia ubora..ni jambo zito sana hapa
Milango iliyofunguliwa na Fursa hii ni mingi, cha ajabu watu ni wagumu kuingia: Fursa hii imefungua milango mingine zaidi ya fursa nyingine. Wanatafutwa watu na makampuni katika utengenezaji wa filamu na muziki. Wapiga picha makiniTanzania. Editors wa filamu bado…akina Diamond Platnum wanakimbilia Afrika kusini kwasababu bado hawajatokea watu makini wa kuishika vizuri sekta hii. Watalaamu katika animations, Mavazi na mapambo kwaajili ya filamu bado. Watengenezaji wa sauti na zaidi. Hizo zote ni fursa ambazo hazijaguswa. Mpaka lini tutaendelea kuuza vibanda na maduka ya vocha wakati kuna wajanja wanatengeneza mamilioni ya pesa katika filamu.
Ernest Napoleon alipokuja Tanzania kwaajili ya kuandaa waandaaji wa filamu yake mpya iitwayo GOING BONGO alihangaika sana kupata waandaaji Tanzania. Alipowaangalia akina Monalisa…akakumbuka uzuri wa filamu ya Girlfriend akadhani viwango vyao vitakuwa vimepanda juu, yaani alichoka mwenyewe alipoangalia filamu za kibongo akakuta viwango ndiyo kwanza vimeshuka kuliko hata filamu ya zamani ya Girlfriend, ikabidi aende Kenya na kurudi Marekani kutafuta watu wengine makini. Aligharamia pesa nyingi sana.
Wapi tumekosea wasanii? Ina maana hakuna msanii mwingine anayeweza kumpindua Kanumba hapa Tanzania? Au kama vipi hiki kizazi cha sanaa kiondoke kiingie kizazi kingine tuikomboe bongo movie?
Filamu zinazotengenezwa kila siku Tanzania ni za viwango vya chini. Yaani ni vichekesho. Akitokea mfanyabiashara makini akafanya kitalaamu na kuwaongoza vijana waigizaji na waimbaji hapa Tanzania, ni Tajiri. Muulize Mkubwa na wanae anavyotamba.
Katika usambazaji ndiyo basi kabisa. Ninawapongeza wasafi kwa kuja na fursa ya kidigitali ambayo tutaiongelea huko baadaye. Unaijua ..www.wasafi.com ….hapa ikiwekwa nguvu tutawasikiliza kwenye mambomba.
Hii ni fursa kubwa zaidi ya maelezo. Ni nani anayeweza kutatua matatizo ya usambazaji wa kazi za sanaa? Ukitafuta njia za kusambaza kazi za sanaa kifaida kama mjasiriamali, wasanii wote watakukimbilia wewe. Unakuwa mfalme
Itaendelea wiki ijayo…
www.fursa101.co.tz
Ingia hapa fanya shopping za bidhaa za kitanzania online:
www.fursa101.co.tz