SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Novemba 2017

T media news

Sio Rahisi Mimi Kupotea Kwenye Game kama Wengine- Ebitoke

UNAMKUMBUKA msanii wa vichekesho aliyejichukulia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Anna Exavery ‘ Ebitoke’, amedai kuwa bado hajapotea kwenye gemu kama wengine wanavyodhani.

Akizungumza na Full Shangwe, Ebitoke alisema kuwa, si rahisi kwa yeye kupotea kwenye gemu kwa sababu amezaliwa kuchekesha, ana madude ya hatari ingawa kwa sasa yuko kwenye majukumu mengine.

“Ha ha ha haaa! Siyo rahisi kupotea kihivyo kama watu wanavyodhani, niko na madude ya hatari sijayaachia, sema kuna majukumu mengine ya kikazi nayafanya,”alisema Ebitoke