MHASIBU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai, anayedaiwa kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.
Gugai amefikishwa katika mahakama hiyo baada ya taarifa iliyotolewa siku chache zilizopita na Naibu Kamishna wa Takukuru, Brigedia John Mbungo, kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ametoroka. Mtuhumiwa huyo anatajwa kumiliki majumba na viwanja karibu kila mkoa nchini.