Imesuniwa kutawadha katika hali nyingi, miongoni mwa hali ambazo muislamu amesuniwa atawadhe:
1. Wakati wa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu
Kwa Hadithi iliopokelewa na Muhaajir bin Qunfudh alimsalimia Mtume na Mtume ﷺ alikuwa akitawadha hakumuitikia salamu mpaka akamaliza kutawadha kisha akapokea salamu na akasema ﷺ:
انه لم يمنعني ان ارد عليك الا اني كرهت ان اذكر الله الا على طهاره] رواه أبوداود وإبن ماجة]
[Haikunuzulia mimi kukuitika salamu ila nilichukia Kumtaja Mwenyezi Mungu ila nikiwa kwenye Twahara] [Imepkewa na Abuu Dawud na Ibnu Maajah]
Ni bora ikafahamika kwamba Bwana Mtume alikuwa akimdhukuru Mola wake katika hali zote, akiwa amekaa au amesimama, akiwa ana udhu au hana, akiifanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu:
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا} الإنسان:25}
[Na likumbuke jina (litaje) la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni] [76:25].
Udhu ni silaha ya muumini, kwa hivyo ni vema saa zote akawa anatembea na silaha yake hiyo, khasa khasa wakati wa kumdhukuru Mola wake.
2. Wakati wa kulala.
Kwa Hadithi iliyopokelewa na Albaraai bin Aazib – Allah amuwie radhi – amesema:
اذا اتيت مضجعك فتوضاء وضوءك للصلاه ثم اضطجع على شقك الايمن ثم قل - اللهم اسلمت نفسي اليك - ووجهت وجهي اليك - وفوضت امري اليك - والجات ظهري اليك - رغبة ورهبة اليك - لا ملجاء ولا منجى منك الا اليك - اللهم امنت بكتابك اللذي انزلت وبنبيك اللذي ارسلت-- فان مت من ليلتك مت على الفطره -- واجعلهن اخر ما تتكلم به-
Aliniambia Mtume ﷺ: [Unapokiendea kitanda chako (unapotaka kulala) tawadha udhu wako wa swala, kisha ulalie upande wa kulia, halafu useme:
ALLAHUMMA INNIY ASLAMTU NAFSIY ILAYKA, WAWAJJAHTU WAJ-HIY ILAYKA, WAFAWWADHTU AMRIY ILAYKA, WA ALJA-TU DHWAHRIY ILAYKA RAGHBATAN WA RAHBATAN ILAYKA, LAA MALJAA WALAA MANJAA MINKA ILLAA ILAYKA. ALLAHUMMA AAMANTU BIKITABIKAL-LADHIY ANZALTA, WABINABIYYIKAL-LADHIY ARSALTA] [Imepokewa na Bukhariy.]
3. Ni sunna kutawadha kwa mtu aliye na janaba anapotaka kula, kunywa au kulala. Imepokelewa kutoka kwa Ammaar bin Yaasir –Allah amuwie radhi kwamba Mtumeﷺ:
[ان النبي صلى الله عليه وسلم رخص للجنب اذا اراد ان ان ياكل او يشرب او ينام ان يتوضاء وضوءه للصلاه]
[Amemruhusu mwenye janaba anapotaka kula, kunywa au kulala atawadhe udhu wake wa swala (ndipo ayafanye hayo yaliyotajwa] [Imeokewa na Tirmidhiy.]
4. Imesuniwa kutawa kabla ya kukoga josho la janaba.
Imepokewa kutoka kwa Bi Aysha – Allah amuwie Radhi amesema : Alikuwa Mtume ﷺ:
اذا اغتسل من الجنابه يبداء فيغسل يديه ثم يفرغ بيمينه على شماله فيغسل فرجه ثم يتوضاء وضوءه للصلاه] رواه البخاري ومسلم]
[Anapotaka kukoga, huanza kwa kuosha mikono (vitanga) vyake, halafu humimina maji kwa mkono wake wa kulia na huukosha utupu wake kwa mkono wa kushoto. Halafu hutawadha udhu wake wa swala,] kisha ndipo hukoga baada yake [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim.]
5. Wakati wa kumbeba maiti.
Kwa Hadithi ilipokelewa na Abuu Dawud na Attirmidhy
من غسَّل ميتاً فليغتسل ، ومن حمله فليتوضأ ] . أخرجه أبو داود والترمذي]
[Mwenye kumuosha maiti akoge na mwenye kumbeba na atawadhe] [Imepokewa na Abuu Dawud na Attirmidhiy]
6. Wakati mtu aghadhibikapo sana,ni suna akatawadhe kwa sababu udhu husaidia kuzima mfumuko na mchemko wa ghadhabu na humrejesha mtu kwenye hali ya utulivu.
Imepokelewa kutoka kwa Atwiyah Al-aufaa kwamba Mtume wa Allah ﷺ amesema :
[إِنَّ الْغَضَبَ مِنْ الشَّيْطَانِ وَإِنَّ الشَّيْطَانَ خُلِقَ مِنْ النَّارِ وَإِنَّمَا تُطْفَأُ النَّارُ بِالْمَاءِ فَإِذَا غَضِبَ أَحَدُكُمْ فَلْيَتَوَضَّأْ]
[Bila ya shaka ghadhabu hutokana na shetani, na huyo shetani amuembwa na moto na bila shaka moto huzimwa na maji. Basi ashikwapo na ghadhabu mmoja wenu na akatawadhe] [Imepokewa na Ahmad na Abuu Dawud.na Isnadi yake ni Dhaifu]
7. Ni suna kujadidi udhu (kutawadha udhu juu ya udhu) kwa kila swala.
Kwa Hadithi ya Bwana Mtume ﷺ:
لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي ، لَأَمَرْتُهُمْ عِنْدَ كُلِّ صَلَاةٍ بِوُضُوءٍ ، ومَعَ كُلِّ وُضُوءٍ بِسِوَاكٍ] رواه أحمد والنسائي]
[Lau si kuwaonea taabu umati wangu ningaliwaamrisha kutawadha kwa kila swala na kupiga mswaki kwa kila udhu.] [Imepokewa na Ahmad na Annasai]
Na Ilikuwa ni ada ya Bwana Mtume Rehema na Amani zimshukie –kutawadha kwa kila Swala na baadhi ya nyakati akiswali