Mfanyakazi katika kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter, ameifunga akaunti ya Rais wa Marekani Donald Trump, @realdonaldtrump, kitendo ambacho kimeelezwa na kampuni hiyo kuwa ni makosa ya kibinadamu yliyofanywa na mfanyakazi huyo.
Earlier today @realdonaldtrump’s account was inadvertently deactivated due to human error by a Twitter employee. The account was down for 11 minutes, and has since been restored. We are continuing to investigate and are taking steps to prevent this from happening again.
— Twitter Government (@TwitterGov) November 3, 2017
Twitter imeeleza kuwa akaunti ya Rais Trump yenye jina @realdonaldtrump iliondolewa jana Alhamisi kwa muda wa dakika 11 na mfanyakazi ambaye alikuwa amebakiza muda mfupi wa kufanya kazi katika kampuni hiyo.
Through our investigation we have learned that this was done by a Twitter customer support employee who did this on the employee’s last day. We are conducting a full internal review.https://t.co/mlarOgiaRF
— Twitter Government (@TwitterGov) November 3, 2017
Kwa sasa akaunti y Rais Trump imesharejeshwa hewani na haikupata madhara yoyote.
Twitter imesema kuwa inachunguza tatizo hilo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kisa kama hicho hakitokei tena.
Rais Trump ambaye ana wafuasi zaidi ya 41 milioni na ni mtumiaji mkubwa wa mtandao wa twitter, hajasema lolote kuhusu kufungiwa kwa akaunti yake.