SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 18 Septemba 2017

T media news

This is Simba and that is Okwinho”-Haji Manara

Kama unavyojua Haji Manara anapenda kutamba hususan pale timu yake inapopata matokeo uwanjani, sasa amekuja na jingine tena baada ya Okwi kuweka kamabani bao mbili Simba ilioifunga Mwadui bao 3-0 Jumapili ya Septemeber 17, 2017.

Manara ameibuka na ku-post mara mbili kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu mshambuliaji wao Emanuel Okwi ambaye kwa sasa amefikisha magoli sita kwenye ligi ikiwa amecheza mechi mbili pekee.

“East Africa ina Okwi mmoja tu, game mbili goli sita, mara mbili ya magoli yote ya Gongowazi kwa game zao tatu!! Kosa lao lilikuwa kumwita mhenga, atashinda kila tuzo nchi hii. This is Simba and that is Okwinho”-Haji Manara.

Sasa Manara hakuishia hapo, katika post yake nyingine inaonesha picha ya mashabiki wa Yanga wakiwa wamevaa jezi ya Okwi enzi hizo akiwa ni mchezai wao lakini kubwa ni ujumbe ulioambana na hiyo picha.

“Kila mtanzania anatamani Okwi aichezee klabu yake, lugha ya picha ndio inavyosema, hahahahahaha!! huyu mhenga noma sana wallahi, ukinuna naleta nyingine.”