SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Septemba 2017

T media news

Sekunde 14 zaiponza Leicester City kwa FIFA

Ulaya hakuna magumashi katika soka, kila jambo linalofanyika nchi za wenzetu linafuata muda na taratibu, hakuna jinsi yoyote unaweza kukwepesha muda au taratibu za soka.

Katika msimu wa dirisha la usajili lililopita klabu ya Leicester City walijaribu kumnunua Adrien Silva kutoka katika klabu ya Sporting Lisbon inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ureno.

Leicester City walifanya kila juhudi siku ya mwisho ya usajili kumnunua kiungo huyo lakini walichelewa kwa muda wa sekunde 14 tu kukamilisha dili hilo lililowagharimu kiasi cha £21m.

Ina maana dirisha lilikuwa likifungwa 00:00 kamili usiku lakini Leicester wenyewe wakafanikisha kumnunua Silva ilipofika saa 00:14 ikiwa ni sekunde 14 baadaye ndipo Leicester walimsaini Silva.

Kutokana na suala hilo FIFA waliamua kuzuia usajili wa Silva huku wakiiacha Leicester City ikipambana kujaribu kukata rufaa ili Adrian Silva aichezee klabu hiyo.

“Tunafanya jitihada za ziada kuhakikisha tunakamilisha suala la Adrien, usajili wake ulishakamilika na tunaamini wenzetu wa Leicester City watatafuta suluhisho la suala hili” alisema msemaji wa Sporting Lisbon.

Leicester City bado wanajaribu kuishawishi FIFA wamruhusu Silva acheze kwani baadhi ya taarifa za kiungo huyo zilitumwa mapema FIFA ila nyingine ndio zilikamilika sekunde 14 baadaye.