SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 7 Septemba 2017

T media news

Ndoa ya Dulla Makabila yaota Mbawa Wazazi Wamkataa Sajent

Ile ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kati ya msanii wa singeli nchini Tanzania, Dullah Makabila na Husna Sajent ambaye ni muigizaji wa bongo movie imeingia dosari baada ya wazazi wa dulla kumkataa mwanamke huyo.

Hayo yamebainishwa na Dullah wakati akizungumza na katika kipindi cha eNewz kutoka EATV na kusema hilo suala ni kweli wala siyo tetesi, huku akidai atajua ni namna gani ya kuyamaliza kwa sababu imani yake ya dini inamruhusu kuoa mwisho wanawake wanne.

"Hayo masuala ni kweli yapo na yameshatokea nyumbani kwa wazazi, tutajua jinsi ya kuyamaliza ila kikubwa ni mtu kuwa katika misimamo yake kwa sababu sisi ni watoto wa kiislamu tumeruhusiwa kuona mwisho wanawake wanne", amesema Dullah.

Pamoja na hayo, Dullah amedai mpaka kutokea wazazi wake kumkatalia kumuoa Husna alikuwa hajafanya jambo lolote la kumchumbia japo aliongea na mshenga wake HK kuhusiana na suala hilo.

"Mpaka dakika hii mimi nipo katika wakati mgumu sana, sema tu watu hawatambui hilo lakini mimi naweza sema sasa hivi nina kipindi kigumu katika kulimaliza hili suala. Nina muomba Mungu aweze kunifanyia wepesi ili niweze kuyamaliza haya masula salama",amesisitiza Dullah.

Kwa upande mwingine, Dullah amesema mpaka sasa hivi hakuna jambo lolote linaloendelea kutoka kwa mshenga wake kwa kuwa alishamwambia yaliyomkuta kuhusu mchumba wake.