Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amekana suala la kutengeneza kiki katika mitandao ya kijamii.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Love You Dia’ aliyoshirikishwa na Patoranking, ameiambia Radio Maisha, Kenya kuwa mitandao yake anaitumia kuwajuza mashabiki taarifa mbali mbali na sii vinginevyo.
“Hamna, mimi kama kwa mfano kwenye Instagram na kwenye mitandao yangu ya kijamii nawapa habari zangu zinazotokea mara kwa mara. Kazi yangu mimi ni ya muziki, kwa hiyo watu wanakuwa wanaburudika,” amesema Diamond.
“Huwa naweka mwenyewe, wapo digital management pale ofisini kwetu lakini ile niwe active sometimes huwa nafanya mwenyewe,” ameongeza.
Diamond katika mtandao wa instgrama ana followers 3.9 milioni, twitter 429k facebook like 2. milioni.