Leo Jumamosi September 16, 2017 ligi kuu Tanzania bara inaendelea kwa mechi tano zitakazochezwa kwenye viwanja tofauti, jana ulichezwa mchezo mmoja Azam 1-0 Kagera Sugar huku kesho ikitarajiwa kuchezwa michezo mingine miwili.
Kati ya mechi zitakazochezwa leo, mchezo wa Majimaji FC vs Yanga ndio utafuatiliwa na mashabiki wengi ukilinganisha na mechi nyingine.
Yanga watakuwa ugenini kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ikiwa ni juma moja tangu wacheze dhidi ya Njombe Mji ya Songea.
Jerry Tegete na Danny Mrwanda
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars aliyetengeneza jina akiwa na kikosi cha Jangwani kwa sasa yupo Majimaji FC hivyo leo atakuwa akicheza dhidi ya timu yake ya zamani.
Tegete aliondoka Yanga baada ya nafasi yake kuwa finyu ndani ya kikosi cha Yanga na muda mwingi kuishia benchi. Alijiunga na Mwadui chini ya kocha Julio ambako pia hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza. Akaondoka zake baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na Majimaji.
Mrwanda aliwahi kuitumikia Yanga baada ya kutoka Vietinam, msimu uliopita aliheza kwenye kikosi cha Kagera Sugar lakini atakuwa akikutana na Yanga kwa mara nyingine akiwa upande wa pili.
Uwanja
Uwanja wa Majimaji ni miongoni mwa viwanja vinavyopigiwa makelele kwa ubovu wake, huenda ukawa kikwazo kingine kwa Yanga kucheza mpira wao wa pasi za chini. Msimu uliopita Yanga walipoteza mechi kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga dhidi ya Stand United halafu wakatoka sare dhidi ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona baadae walivilalamikia viwanja hivyo kuwapa ugumu kupata matokeo.
Mechi 4 Majimaji aijapata ushindi kwa Yanga
Katika mechi nne zilizopita za ligi kuu Tanzania bara Majimaji haijafanikiwa kuifunga Yanga hata mara moja, wamefungwa mechi tatu na kuambulia sare katika mchezo mmoja.
16/06/2017 Majimamaji ?? Yanga
17/01/2017 Majimaji 0-1 Yanga
10/09/2016 Yanga 3-0 Yanga
21/05/2016 Majimaji 2-2 Yanga
21/01/2016 Yanga 5-0 Majimaji
Nafasi ya Yanga, Majimaji, kwenye ligi
Yanga ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi nne baada ya mechi mbili wakati Majimaji wao wakiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi yao moja baada ya mechi mbili.
Majimaji bado haijashinda msimu huu, imecheza mechi mbili imepoteza mchezo mmoja na kupata sare mchezo mwingine (Mbeya City 1-0 Majimaji, Prisons 2-2) Majimaji. Yanga ilitoka sare mechi yake ya kwanza halafu imeshinda mchezo mmoja (Yanga 1-1 Lipuli, Njombe Mji 0-1 Yanga).