SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 15 Septemba 2017

T media news

Juma Nyoso anarudi tena Azam Complex, matukio mengine makubwa Azam vs Kagera Sugar

Azam FC vs Kagera Sugar ni bonge la mechi kwa siku ya leo, mechi pekee katika ratiba ya VPL itakayochezwa leo Ijumaa September 15, 2017 kwenye uwanja wa Chamazi kuanzia saa 1:00 usiku.

Mechi hii ina mambo mengi ya kuangalia lakini ShaffihDauda.co.tz imeangazia mambo makubwa matatu yanayoufanya mchezo huu kuwa wakuvutia kuushuhudia. Kumbuka Juma Nyoso anarejea Azam Complex kwa mara ya kwanza baada ya kucheza mechi yake mwisho  kwenye uwanja huo iliyopelekea kufungiwa.

Mbaraka Yusuph atakuwa akicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar tangu aliposajiliwa na Azam FC akitokea Kagera Sugar. Kuna kinda mwingine wa Kagera nay eye ametokea Azam U20 atakuwa akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Azam baada ya kujiunga na Kagera Suga.

Ozuka Izechuku

Kijana mwingine raia wa Nigeria atakuwa akikutana na Azam timu yake ya zamani ambayo alikuwa akiitumikia katika kikosi cha vijana wa U20, amekaa sana Chamazi na anajua udamaduni wote wa Azam.

Kwa sasa anafanya vizuri akiwa na Kagera Sugar, timu ya Kagera Sugar inautamaduni wa kutoa man of the match kwa mechi zao wanazocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani Kaitaba. Mechi yao ya kwanza kwenye ligi ambayo walifungwa 1-0 na Mbao FC kijana huyu alichaguliwa na mashabiki kuwa man of the match wa mchezo huo.

Kwa hiyo Ijumaa ya September 15, 2017 anarudi tena Chamazi akiwa upande wa pili na atakuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wanaliandama goli la Azam kama ilivyokuwa kwa John Bocco, Erasto Nyoni na Aishi Manula wakati Azam ilipocheza na Simba juma lililopita.

Mbaraka Yusuph Abeid

Atakuwa akikutana na timu yake ya zamani iliyompa jina baada ya kupewa nafasi na kocha Mecky Mexime jamaa alifanya kweli kwa kupachika mabao ya kutosha na kuwafanya matajiri wa Azam kuamua kumsajili kwenye kikosi chao.

Baada ya kufanya vizuri akiwa na Kagera Sugar aliitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Botswana pamoja na Burundi.

Ni hawahawa Kagera Sugar waliomfanya Mbaraka akashinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi ligi kuu Tanzania bara 2016/2017, lakini leo atakuwa akipambana kuifunga Kagera Sugar ili kuipa pointi tatu timu yake ya sasa Azam FC.

Juma Nyoso

Kama unakumbuka vizuri Juma Nyoso alicheza mechi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Azam kabla ya kufungiwa miaka miwili kucheza soka September, 2017 kwa kitendo cha kumdhalilisha John Bocco ambaye wakati huo alikuwa bado yupo Azam. Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Chamazi wakati wa mchezo kati ya Azam vs Mbeya City.

Nyoso leo anarudi kwenye uwanja wa Chamazi uwanja wenye kumbukumbu mbaya kwake kwa sababu baada ya mechi hiyo hakucheza tena ligi kuu  akiwa nyumbani anatumikia adhabu yake, inawezekana uwanja huu ukawa ni miongoni mwa viwanja ambavyo vimekaa kwenye kumbukumbu mbaya za Nyoso.