SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 17 Septemba 2017

T media news

Canelo Alvarez na Gennady Golvkin hakuna mbabe

Asilimia kadhaa ya watu waliotazama pambano kati ya Conor McGregor na Floyd Mayweather waliliponda sana pambano hilo, wengi walidai yalikuwa maigizo na watu hawakuwa serious kuhusu ngumi ilikuwa upigaji.

Usiku wa kuamkia leo nchini Marekani kumepigwa pambano moja matata sana ambalo wafuatiliaji wengi wa masuala ya masumbwi walikuwa wakulisubiri kwa hamu na kuamini hili ndio pambano haswa la ngumi.

Canelo Alvarez alivaana na Gennady Golvkin katika uwanja wa T Mobile nchini Marekani katika pambano ambalo ngumi zilipigwa sana lakini hadi mpambano unamalizikia hakukuwa na mbabe kwani majaji waliamua sare.

Pambano ambalo kila mshabiki aliona bondia wake anashinda kutokana na makonde yalivyosukumwa lakini majaji Adalaide Byrds akimpa Alvarez point 118-110, Dave Merrotti akampa Golvkin 115-113, huku Don Trella akiamua sare ya kwa kuwapa 114 kwa 114.

Mashabiki 22,358 waliojitokeza walitaraji kuona knock out ikitokea kutokana na ngumi zilivyokuwa zinapigwa lakini mwisho wa siku waliona Golovkin akibaki na mikanda yake ya WBC,WBF na WBO katika ngazi ya middleweight.