Linapokuja suala la kuangalia ni Application gani zilizopakuliwa zaidi na watumiaji wa simu za Android kwa mwezi uliopita, bado kampuni ya Facebook na kundi lake linaongoza kwenye kinyang’anyiro hiki kisicho rasmi. Kama inavyoonekana kwenye chati ya Statistica, kampuni ya Facebook inaongoza kwa mbali sana kwa watumiaji wa simu za Android. App nne zilizopakuliwa zaidi zote zinamilikiwa na kampuni ya Facebook. Zikijumuishwa, app hizi za kampuni ya Facebook zimepakuliwa mara milioni 297 kwa mwezi uliopita peke yake.
Kwa mujibu wa “Priori Data,” WhatsApp ndiyo iliyoongoza kwa kupakuliwa mara milioni 103.64. Kampuni ya Facebook iliinunua app hii ya kutumiana ujumbe mwezi Februari mwaka 2014 kwa gharama ya dola bilioni 19 (zaidi ya shilingi trilioni 42.5). Toka kununuliwa mwaka huo, app hii imekuwa ikipata umaarufu zaidi na zaidi.