Kila mmoja wetu anaona jinsi ambavyo Mh. rais, Dkt Magufuli anavyofuata utawala wa sheria na katiba yetu pendwa. Pamoja na kuwa asilimia 100 ya watanzania tunataka awe rais wa kudumu, ila yeye Mh. rais alishalitolea ufafanuzi kuwa atafuata katiba inasemaje, yaani urais ni miaka 10 tu.
Pamoja na kuwa kwa nchi yetu haijawahi kutokea mtabiriwa wa urais kuwa rais, mfano, Mh. Dkt JK alidhaniwa 1995, lakini akaibuka Mh. Mkapa, na 2015 alidhaniwa Lowassa/Membe ila akaibuka Mh. Dkt Magufuli.
Je kwa 2025 nani anaweza kushika mikoba?