SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

T media news

Lipuli imekuwa timu pekee iliyopata pointi kati ya zilizopanda daraja 2017/18

Lipuli FC ndio timu pekee ambayo imeambulia pointi kati ya timu tatu ambazo zimepanda daraja msimu huu, sare ya kufungana 1-1 na Yanga kwenye uwanja wa Uhuru imewapa Lipuli pointi moja ugenini katika mechi yao ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara 2017/2018.

Bao safi la Seif Abdallah Karihe alifunga goli zuri la kuongoza kwa Lipuli FC lakini Donald Ngoma akasawazisha kwa upande wa Yanga kwa kuunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Juma Abdul.

Sare ya kufungana 1-1 na Yanga imeipa Lipuli pointi moja ya ugenini na kuwa timu pekee kuambulia pointi kati ya zilizopanda daraja msimu huu ambapo timu nyingine zilikumbana na vipigo.

Katika timu tatu ambazo zimepanda daraja msimu huu, mbili kati ya  hizo (Singida United na Njombe Mji) zimepoteza mechi zao za kwanza kwenye ligi. Singida United wakiwa ugenini mkoni Shinyanga, walichezea 2-1 kutoka Mwadui FC kwenye uwanja wa Mwadui Complex wakati Njombe Mji wao walikula kichapo cha 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Wakati watu wakijiandaa kushuhudia mzunguko wa mechi za pili, ligi itasimama kwa muda kupisha wiki ya mechi za kalenda ya FIFA ambapo timu ya taifa ‘Taifa Stars’ itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana  September 2, 2017 na tayari wachezaji wanaoounda timu ya taifa wameshaitwa kambini kwa ajili ya maandalizi.