SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

T media news

Kimbunga Harvey: Watu 2,000 waokolewa kutoka kwa mafuriko Houston, Marekani Saa 3 zilizopita

Maafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyakeHaki miliki ya pichaREUTERS

Maafisa karibu 3,000 wa idara ya kulinda bahari wanasaidia katika uokoaji Houston na viunga vyake
Watu takriban 2,000 wameokolewa kutoka kwa mafuriko katika mji wa Houston na viunga vyake, huku kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa sana maeneo ya jimbo la Texas.
Kumekuwa na ripoti za kutokea kwa vifo pamoja na magari kadha kuzidiwa na nguvu za maji.
Hata hivyo, uchunguzi bado unaendelea, afisi ya liwali mkuu wa wilaya ya Harris, Darryl Coleman amesema.

Gavana wa Texas Greg Abbott ameambia wanahabari kwamba hawezi kuthibitisha vifo vinavyodaiwa kutokana na mafuriko hayo.
Vimbunga vinavyopewa majina duniani
Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali ambayo inashuhudiwa katika eneo hilo haijawahi kushuhudiwa awali.
Idara hiyo imesema kulitokea mafuriko ya ghafla eneo la katikati mwa mji wa Houston, na uchukuzi umetatizika.
Vyumba vingi vya kutoa hifadhi wakati wa majanga vimefunguliwa, ukiwemo ukumbi mmoja wa mikutano.
Gavana Abbot amesema barabara karibu 250 zimefungwa Texas na kwamba ameiomba serikali kuu itangaze janga katika wilaya 19, ombi ambalo limeidhinishwa na Rais Donald Trump.
"Tutaendelea kupokea mvua kubwa," amesema gavana huyo