SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 15 Agosti 2017

T media news

Breaking: Mke wa Rais Mugabe ajisalimisha Polisi

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe amejisalimisha mikononi mwa  Jeshi la Polisi nchini Afrika Kusini akikabiliwa na shtaka la kumshambulia msichana mmoja mwenye miaka 20 baada ya kumkuta hotelini akiwa na wanawe wawili wa kiume.

Waziri anayehusika na masuala ya Polisi nchini Afrika Kusini amewaambia waandishi wa habari kuwa mke huyo wa Rais wa Kwanza wa Zimbabwe hayupo chini ya ulinzi kwa sababu alijisalimisha na kuonyesha ushirikiano vizuri.

Grace anatuhumiwa kumjeruhi msichana kwa kutumia waya wa umeme ambapo kwa mujibu wa jumbe msichana huyo alizochapisha katika akaunti yake ya Twitter, alishambuliwa wakati walinzi wakitazama bila kutoa msaada.

Mke wa Rais Mugabe awafumania wanawe na kumshambulia msichana aliyekuwa nao

Msichana huyo, Gabriella Engels alisema alikuwa amewatembelea watoto wa Mugabe, Robert Jr na Chatunga na mama yao alipomkuta akawatoa wanawe na kuanza kumshambulia.

Gabriella alifafanua kwamba, mama yao alimtuhumuwa kuwa amekuwa akiishi na  watoto hao ambapo wapo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo.

Gabriella alisema tangu kutokea kwa tukio hilo hakuwa amepigiwa simu na watoto wa Mugabe ambao ni rafiki zake.

Pia alisema yeye ni mwanamitindo lakini kutokana na jeraha alilopata usoni hajui ataweza kuendelea na kazi hiyo.

Mke wa Mugabe amefikishwa mahakamani leo mchana kujibu tuhuma za kushambulia na kumjeruhi msichana huyo.