Usiku wa August 17, 2017 Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege ikiwa ni mechi ya kujipima kwa upande wa ‘mnyama’ kuelekea pambano la watani wa jadi la Ngao ya Jamii August 23.
Simba ilibanwa na kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar. Baada ya matokeo hayo, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kikosi chao bado kinakabiliwa na tatizo la umaliziaji.
“Ushambuliaji na umaliziaji pakeake ndio bado tuna shida hapo lakini bado tunajaribu kurekebisha hapo,” – Jackson Mayanja, kocha msaidizi Simba.
Mayanja amewatoa hofu mashabiki wa Simba kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
“Mpira hautabiriki, unaweza ukawa unafunga goli moja au haufungi kabisa lakini siku hiyo unaweza kuona mtu anafungwa tatu au magoli zaidi ya mawili kila kitu kinawezekana kwenye mpira. Mashabiki wa Simba wasipate wasiwasi na mechi hiyo nadhani kila kitu kitakuwa sawa.”