SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 13 Agosti 2017

T media news

Aliyekuwa Mke wa Barnaba Afunguka nini Alikuwa Anakosa Kwa Barnaba Mpaka Kukimbia Ndoa.....

Aliyekuwa mke na mama mtoto wa mwanamuziki Barnaba Elias, Zuu Namela, ametoa kile kinachoitwa la moyoni, na huenda ndio sababu iliyomtoa kwa mzazi mwenzake na kuanzisha mahusiano mapya.
 
Kwenye ukurasa wake wa instagram Zuu Namela ameandika ujumbe kuwa kwa miaka mitano (ambayo ilikuwa ndani ya mahusiano na Barnaba) alikuwa anakosa furaha ya kweli na amani ya moyo, lakini sasa ameipata furaha hiyo baada ya kuachana.

"Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano ichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIyaMOYO " aliandika Zuu Namela.

Hivi karibuni Zuu Namela ameonekana akimpost mwanaume mwengine kwenye ukurasa wake, huku akiandika jumbe mbali mbali za mapenzi, na kuacha mashabiki wake kuwa ndiye mbadala wa Barnaba ambaye ni baba mtoto wake.