Beki wa zamani wa Simba Abdi Banda usiku wa Jumanne August 22, 2017 ameiokoa timu yake Baroka FC kuchapwa kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kufunga bao la kusawazisha.
Banda alifunga goli dakika ya72 akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Sipho Moeti. Goli hilo ni la kwanza kwa Banda tangu ajiunge na Baroka FC akitokea Simba.
Katika mchezo huo, Banda alianza kwenye kikosi cha kwanza na kucheza kwa dakika zote 90.
Sare hiyo inaifanya Baroka kuwa na pointi mbili baada ya kucheza mechi mbili (mechi zote wametoka sare) na wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ya Afrika Kusini (Absa Premiership).