Iwapo unatafuta kazi inayoendana na taaluma au uwezo wako au una shauku tu ya kutaka kujua aina ya ajira zinazotoweka kwenye jamii, tumeweza kupata jumla ya ajira za aina sita zenye uwezekano wa kutoweka na kutokuwa miongoni mwa fursa za ajira baada ya miaka 10. Mabadiliko ya teknolojia na tamaduni zetu yameleta fursa mpya za ajira na kusababisha zilizokuwapo awali kutokomeza kidogo kidogo. Hizi ni aina hizo 6 za ajira zenye uwezekano wa kutoweka:
Watoa huduma za fedha kwenye mabenki
Kwa ongezeko kubwa la huduma za kifedha za kujihudumia mwenyewe kama mashine za ATM, huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu za mkononi pamoja na matumizi ya kadi za benki kwenye maduka wakati wa kununua huduma au bidhaa madukani, wafanyakazi wa benki wanaohudumia wateja wanaoweka au kutoa fedha yanaanza kutoweka kwenye soko la ajira duniani. Teknolojia imewezesha maendeleo makubwa ya jinsi tunavyofanya manunuzi, and customers are wanting less human interaction.
Shughuli za masoko (kutafuta wateja) kwa kutumia simu
Siku hizi watu hawatumii simu kufanya shughuli za masoko ya kampuni kama ilivyokuwa awali. Kwa kutumia njia nyingine za mawasiliano zenye matokeo bora zaidi – kama matumizi ya email au kutuma ujumbe wa maneno, njia ya kizamani ya kutafuta masoko kwa njia ya simu (telemarketing) imeanza kuwa ni kazi ya kizazi kilichopita. Kwa ongezeko la kutafuta masoko kwa njia ya email, kazi hizi ambazo zamani zilikuwa zimezoeleka kuwa ni za uhakika hazitakuwapo sokoni tena.
Uwakala wa safari
Kwa jinsi teknolojia ya intaneti ilivyoshika kasi na uwezo wa mtu kufanya mipango ya safari kwa bei rahisi ukilinganisha na gharama za kutumia mawakala wa safari, kazi hizi zimeshakuwa za kizamani mpaka sasa na taratibu zimeanza kupotea kwenye soko la ajira duniani. Siku za kuhitaji mtu mwingine akusaidie kupata gharama nafuu za ndege unapotaka kusafiri zimekwisha kwa sababu teknolojia ya intaneti imefanya kazi hiyo kuwa rahisi kabisa kwa msafiri.
Udereva wa taxi
Kwenye simu za kisasa (smartphones) kuna ‘application’ nyingi zimeleta mazoea mapya kabisa ya jinsi mtu anavyoweza kupata taxi kwa urahisi na abiria kuweza kuchangia usafiri. Kuita taxi sasa imekuwa ni kazi rahisi kabisa unayoifanya kiganjani kwako ambapo huna hata haja ya kumpigia simu dereva. Ni kitendo cha kuiagiza kwa kumtumia ramani ya sehemu ulipo na yeye kuja moja kwa moja kukuchukua – bila kuongea hata mara moja! Madereva wa taxi wanatakiwa kuendana na kasi hii ili kuweza kubaki kwenye biashara.
Uchapaji
Si jambo la kushangaza kuona kwamba magazeti kwa kiasi kikubwa yamepoteza nguvu yake ya ushawishi iliyokuwa nayo awali kama chanzo cha habari kwa watu. Watu wengi sasa wameamua kutumia teknolojia ya digitali kwenye kupata habari hasa zile za papo kwa papo na habari za burudani na michezo. Makampuni ya uchapaji yamekumbwa na wakati mgumu kuendana na muda kwakuwa kila gazeti la siku linapotoka, habari iliyoandikwa inakuwa si habari tena. Makampuni haya taratibu yanaondoka na kuacha fursa kwa makampuni mapya yanayoweza kuendana na kasi ya teknolojia ya digitali.
Mashirika ya posta
Kukua kwa teknolojia kulikoongeza matumizi ya mawasiliano kwa njia za papo kwa hapo kama huduma za kutumiana ujumbe kupitia mitandao ya kijamii na email. Huduma hizi zimesababisha uhitaji wa huduma zinazotolewa na mashirika ya posta kupungua kidogo kidogo kwa miaka kadhaa sasa. Pia, ongezeko la makampuni binafsi yanayotia huduma kama za mashirika ya posta, mashirika haya ya serikali ambayo yamekuwa ni miongoni mwa waajiri wakuu kwenye nchi nyingi yanakuwa na nafasi ndogo sana kiushindani.