Na Zainabu Rajabu
BEKI wa Yanga, Vincent Bossou kwa sasa ana ofa nne mkononi lakini mwenyewe ameibuka na kusema kuwa tatu kati ya hizo ndizo amezipa kipaumbele.
Bossou ambaye amekwenda Dubai kwa mapumziko ya Siku 10, amethibitisha kupokea ofa nne kutoka Singida United ya Tanzania na timu 3 za Ulaya.
“Nimepata ofa nchi tatu, kama mambo yataenda vizuri nikitoka Dubai nitaunganisha kwenda Uturuki kufanya mazungumzo ila kwa sasa siwezi kukutajia kwa sababu bado mapema sana,” alisema Bossou.
“Kwa Tanzania nimepata ofa Singida United, wenyewe wako tayari kunipa fedha nzuri, ikiwemo dau la usajili na mshahara mnono, hivyo mambo yakiwa magumu nitarudi kuwasikiliza.”
Iwapo dili la kwenda Ulaya likishindikana Vicent Bossue ataungana na kocha wake wa zamani Hans van Pluijm ambaye kwa sasa ndio kocha mkuu wa timu ya Singida United.