SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 12 Juni 2017

T media news

Spika Ndugai Apigilia Msumari Ripoti ya Madini

"Hakuna kitu kibaya kuwa katikati ya dhiki ambayo hukuistahili"-amesema Spika Ndugai baada ya kukabidhiwa ripoti ya pili ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza sakata la mchanga wa Madini Leo Ikulu Jijini Dar es salaam

"Haya ni mambo ya ajabu, ni mikataba ya kijinga na ya hovyo, Mimi na wabunge wenzangu wote kuhakikisha sheria zote zitakazoletwa tutazitendea haki"- Alisema Spika Ndugai

Hatua hiyo imefuata baada ya Mapendekezo ya kamati ya hiyo iliyotaka sheria za nishati Madini zifanyiwe marekebisho ya haraka, ambapo Rais Magufuli ametaka bunge lifanye haraka iwezekanavyo.