Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ataunda timu yake itakayofuatilia suala la madini ya almasi.
Ndugai ameyasema hayo leo baada ya kamati ya pili kutoa ripoti yake kuhusu mchanga wa madini katika makontena 277 yanayoshikiliwa.
Amesema kwa kushirikiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni kiongozi wa shughuli za bunge, watasaidiana kuunda timu hiyo ili kumsaidia Rais katika masuala ya madini.
“Kwa pamoja, rais ukienda huko na sisi tukienda huku, tutafika
Tayari Spika alishaunda kamati kuchunguza suala la madini ya Tanzanite.