Tarehe 2 December mwaka 2010 kamati ya FIFA iliipa nchi ya Russia uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018, uenyeji huu wa Russia katika kombe la dunia ulikuwa ukiipa pia nafasi ya uenyeji wa michuano ya Confedaration Cup inayoanza tarehe 17 June 2017 hadi tarehe 2 July 2017.
Confedaration Cup yenyewe inashirikisha mabingwa wa kila bara pamoja na timu mwenyeji na michuano ya mwaka huu ya Confedaration Cup itakuwa ni michuano ya 10 ikishirikisha timu 8 kutoka katika mabara 6 huku miji ya Saint Petersvurg,Moscow,Kazan na Sochi ikitarajiwa kupigwa baadhi ya michezo.
Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Urusi kuandaa michuano hii lakini kwa bara la Ulaya haitakuwa mara ya kwanza bali ni mara ya tatu kwa bara hili kuandaa michuano ya Confedaration Cup.
Ukiacha timu ya taifa ya Urusi ambayo wenyewe wameingia moja kwa moja kutokana na uenyeji wo katika kombe hili, mataifa mengine yameingia kutokana na kutwaa ubingwa wa bara lao na Cameroon watatuwakilisha Waafrika huku timu ya taifa ya Ujerumani wanakwenda katika michezo hiyo kama bingwa mtetezi wa kombe la dunia.
Kama kawaida michuano hii huwa inachezwa katika hatua mbili ambapo kwanza inakuwa makundi mawili ya timu nne nne ambapo kila timu hucheza fainali na washindi wawili wa mwanzo hupata tiketi kwa ajili ya kwenda katika hatua ya mtoano wa nusu fainali na kisha washindi watakwenda kucheza fainali.
Zimesalia siku 5 tu kwa fainali hizi kuanza kupigwa na yapo mambo muhimu na ya kuvutia kuhusu michuano hii endelea kukaa hapahapa katika website hii kwani kila siku tutakupa taarifa muhimu ambazo zinahusiana na michuano hii ya Confedaration Cup kwa mwaka huu 2017.