SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 4 Mei 2017

T media news

WAJUE 'YAKUZA' Genge Hatari Zaidi la Kihalifu Japan Lililosambaa Duniani Kote..!!!


Leo nimeona tuwajadili kwa undani kundi kubwa kabisa la kihalifu la kijapani na barani Asia liitwalo YAKUZA

Naamini humu kuna watu wanawajua zaidi yakuza hivyo kile kidogo ambacho ninachokijua kuhusu hawa jamaa nitakiweka hapa na wewe chochote unachokijua kuhusu hawa jamaa kiweke hapa unifaidishe mie na wengine

Binafsi katika elimu hii ya Organised Crimes watu hupenda kuwaongelea MAFIA kama ndio mabingwa wa Organised Crime na kuwasaahau kwa undani sana Yakuza

Yakuza ni genge la kihalifu ambalo chanzo chake ni japan ikikadiriwa kuwa na watu zaidi ya laki moja na elfu tatu

I03,000 na wako duniani kote hawa members wao wamesambaa mabara yote duniani kuanzia Asia, Ulaya, Amerika na Africa yetu hii

Genge hili halikuanza leo ila limeanza tokea mnamo karne ya 17

Hawa majamaa kazi zao sana sana ni Kufanya biashara haramu zote unazozijua wewe pamoja na kufanya shuguli zingine za kihalifu

Hawa majamaa unaambiwa wakitaka roho yako wanakuja kuichukua hata ukiwa umejifungia kwenye chumba cha IGP Mangu

Kwani inasemekana Yakuza Assasins Team ni watu ambao ni proffesional trained NINJITSU members

Ninjitsu ni staili au aina ya martial arts ambayo uki quilify unaitwa NINJA ambaye nina uhakika kwa asilimia mia moja hakuna polisi yeyote wa Mangu anaweza kuwazuia NINJA Assasin Team

Hawa yakuza wanapatikana sana Japan ambapo ndio Origin yao hasa kwenye kisiwa kimoja kinaitwa

KYUSHU

Adhabu zao

Yakuza mmoja akifanya kosa huwa anapata adhabu kama ifuatavyo

Akifanya kosa la kwanza adhabu yao ni kukatwa kidole

Utawajuaje Yakuza

Yakuza wengi hupenda kujichora Tatoo mwili mzima 

Kwani tatoo zao ni ishara ya wao kujuana

Hasa wakiwa wanacheza Oicho-Kabu (oicho-kabu ) ni mchezo wa card kama vile baccarat and blackjack huwa wanavua mashati yao ili kujuana kusudi kujikinga na maadui zao ambao huwa wanaweza kujipenyeza kwenye mchezo huo kwa lengo tu la kusaka information

Kama Mafia na Yakuza wana Crime families ambazo ni

Yamaguchi Gumi

Hii ndio familia kubwa zaidi kwa yakuza yenye members asilimia 50 ya yakuza wote

Sumiyoshi Kai

Hii ina members zaidi ya 20,000 wa yakuza

Inagawa Kai

Haka ndio kadogo yenye members zaidi ya 15,000

Na Headquater ya yakuza ni FUKUOKA headquater huwa zinabadilishwa kutokana na upepo unavyoenda ila tokea waichague mwaka 2008 hawajabadilisha tena na mpaka sasa fukuoka Japan ndio inatajwa kuwa ndio Headquater ya Yakuza

Ila hata hivyo wamesambaa sana miji mingine ya japan kama

Tokyo, kumamoto, hiroshima, kyoto, hyogo pamoja na Aichi

Mitaa yao inajulikana kwa wakazi wa Tokyo inajulikana kabisa kuwa mitaa ya Shinjuku ndio ngome kuu ya kujidai kwa yakuza I mean ndio viwanja vyao ila nani sasa aende kuwakamata

Hakuna mtu si polisi, si mamlaka ya usalama na vyombo vya usalama wa japan vinavyothubutu kupeleka pua zao kule

Kwa marekani YAKUZA wanapatikana sana Hawaii vile vile wanapatikana sana miji ya Denver, New York, Huston na Oregon

Hakuna anayemjua Bosi wa Yakuza sura yake haijawahi kuonekana na wala hakuna mtu ambaye alishakutana nae

Hata hivyo sura pekee wa bosi wa yakuza kuoneshwa ni bwana Shinobu Tsukasa yeye ndie bosi mkuu wa familia ya YAMAGUCHI.. ambayo ndio familia kubwa sana ya YAKUZA huyu jamaa yeye na mabosi wengine wa familia zingine zinaripoti kwa bosi mkubwa ambaye anabaki kutokujulikana na mtu yeyote