SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 16 Mei 2017

T media news

UVCCM: Ndoto za Lowassa ni Sawa na za Mfu..!!!


Na Mwandishi Wetu,

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umemtaka Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowassa kufuta fikra na ndoto mfu za kudhani chadema kama kina misuli ya kukibwaga chama tawala hata kama kitatumia mgongo wa UKAWA.

Umesema upizani nchini hawajawa na jeuri ya kuishinda CCM kwa kuwa hawajafanya mandalizi yoyote ya kweli kumudu kuendesha dola, licha ya kupita karibu miaka 25 yangu Tanzania ilipojiunga na mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Pia Umoja huo umeponda hesabu za Lowassa kwamba CCM inaweza kuondolewa madarakani kwa muungano upinzani aidha kuungana, kusimamisha mgombea mmoja katika kila jimbo na nafasi ya urais au kutogombana wenyewe kwa wenyewe.

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka siku chache baada ya Lowassa kutoa matamshi yaliodai ccm mwaka 2020 inaweza kupulizwa kwa upepo kama inzi anavyotolewa kwenye bilauli la maziwa.

Shaka alisema kwa bahati mbaya Lowassa amesukumwa na hasira na kujikuta akajitoa CCM mwaka 2015 kama mtu aliyekuwa anacheza tombola kwa kuota huenda angeukwaa urais huku yeye mwenyewe akijua fika upinzani ni dhaifu, hauna malengo. mipango wala mikakati ya kushinda uchaguzi .

Alisema kama kuna kosa ambalo Lowassa amelifanya ni kuhama ccm na kujiunga upinzani hasa chadema kwasababu yeye mwenyewe ameshawahi kutamka hadharani akihutubia mkutano wa hadhara huko Mto wa mbu mwaka 2006 akiulinganisha upinzani na watoto wanaokimbilia mdundiko.

"Lowassa asikubali kucheze tombola katika siasa, siasa ni hesabu na fomula zake,nafikiri amekurupuka kujiondoa ccm, ameupanda mkenge kwenda chedema , ajue si Ukawa wala udeta wenye ubavu wa kuiondosha CCM madarakani "Alisema Shaka.

Alimtaka Lowassa kujua kuwa hata viongozi na wanachama wa upinzani hawamuafiki mwanasiasa huyo kwa asilimia kubwa kwani wapo viongozi aliowakuta ambao wametoa jasho jingi kuvijenga vyama vyao hivyo hawako tayari kumpiisha agombee urais au Waziri mkuu wa zamami Frederick Sumaye .

Akijibu hoja na madai yaliotolewa na Lowasa aliyesema kuna ukandamizaji wa demokrasia, Shaka alisema haiba ya demokrasia iliopo Tanzania huwezi kukutana nayo mahali popote Afrika, Afrika Mashariki na duniani ila uamuzi wa serikali ya awamu ya tano ni kuwahimiza wananchi kufanyakazi na kuzalisha mali viwandani na mashambani .

"Uhuru, demokrasia au watu kujitawala bila shibe na maendeleo ya kisekta ni upuuzi, tumemaliza kampeni na uchaguzi mkuu kila mmoja sasa afanye kazi, kukusanya watu kwenye makongamano na kuwapa bahashish ni kuwapumbaza kiakili ikiwa bado ni masikini "Akieleza

Aidha Kaimu Katibu Mkuu alibainisha kuwa anachokieleza Lowassa akimshutumu Rais Magufuli eti kwanini hakwenda Arusha kushiriki maombolezo ya vifo vya wanafunzi . Shaka alisema kushiriki kwa viongozi wa serikali akiwemo na Makamo wa Rais ni uwepo wa Rais na taji la utawala wake

Alieleza Serikali yoyote ni taasisi pana yenye mikono mingi ya kiutendaji ambayo kwa kadri itakavyofanya na kutenda hutimiza yote kwa niaba ya hadhi ya nafasi ya Rais hivyo hakuna mantiki yoyote viongozi wa nchi kukusanyana mahali pamoja kama utitiri au kundi la nzige.

"Akifika mahali popote mteule wa Rais na wateule wengine mwa mintaraf ya uwakilishi huwakilishwa Rais na madaraka yake, Rais hawezi kuwa kama mungu wa madhehebu fulani mwenye mikono saba, vinginevyo Lowassa aseme alihitaji nini Rais afike mahali hapo "Akieleza .

Hata hivyo mtendaji huyo wa UVCCM

alisema mikutano ya hadhara, makongamano, semina au warsha haziwezi kutatua kero na matatizo yanawayowakabili wananchi kiuchumi, kisiasa na kiumasikini bila wananchi wenyewe kuhimizwa pia kujituma

kuzalisha .

Shaka alisema Lowassa na wenzake wana hofu kubwa na kasi ya utendaji wa Rais Dk John Magufuli kwani katika kipindi cha mwaka mmoja na ushee serikali yake imeonyesha maajabu kama iliongia madarakani miaka 10 iliopoita.

"Linalompa kiwewe Lowassa na washirika wake tunalijua, walifikiri Rais Magufuli angeshindwa kuongoza Taifa,

wanashuhudia maajabu ambayo hawayakuyategemea, wanapaparika na kuzua, iko wapi njaa, mahali gani ilipo, nani amekufa kwa njaa, tunasema si chadema, Sumaye wala Lowassa hawawezi kumyumbisha Rais Magufuli"Alimaliza Shaka