SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 4 Mei 2017

T media news

MBARONI kwa Kukutwa na Fuvu la Binadamu..!!!


Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa Kibiti kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha  binadamu.

Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani,  Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa  mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji ya Jaribu.

Lyanga amesema watuhumiwa hao waliokuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kwa kutumia pikipiki  walikuwa wameficha fuvu hilo kwenye begi.

Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki  walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.

Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.