Na Thadei Ole Mushi
Pichani ni Mwanajeshi Mkakamavu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Waziri wa Zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akionekana Mtanashati katika Vazi lake la Uspika wa Bunge la Afrika Mashariki.
KINANA NI NANI
Picha hii ya Kinana ilipigwa wakati Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, nafasi ambayo aliishika kwa Muda wa Miaka mitano.
Mafanikio ya Kinana.
Kinana anatajwa kuwa Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi wa Mwaka 1995 uliomuingiza Madarakani Rais Benjamin William Mkapa na pia Mwaka 2005 na 2010 katika Uchaguzi Mkuu uliomuingiza Madarakani Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Kinana pia ameshiriki kama mwenyekiti wa kamati iliyomwingiza madarakani Mh Magufuli 2015.
Kinana anatajwa kama Meneja Kampeni aliyepata mafanikio makubwa zaidi kwenye kampeni za CCM toka mfumo wa vyama vingi kurudishwa nchini 1992. Pia kinana namuona kama katibu mkuu aliyepata mafanikio makubwa zaidi ya watangulizi wake.
Kinana kama katibu Mkuu wa chama aliweza kuzunguka Tanzania nzima akisikiliza kero za wananchi na kuisimamia serikali. Mpango huo umeonekana kukiimariasha zaidi chama cha mapinduzi na kukisogeza karibu zaidi na wananchi.Ndie aliyekitoa chama kwenye ofisi na kukipeleka kwa wananchi, ndiye aliyeacha kukisimamia chama kwenye makaratasi na kwenda kukisimamia field.
Kinana ni mtu mwenye msimamo sana japokuwa huonekana mtulivu hasa wakati wa kuongea.
Yeye ndiye muasisi wa dhana ya mawaziri mzigo na amekuwa akitoa msukumo mkubwa sana kwa serikali kuwashughulikia mawaziri na watendaji wazembe.
Kama mtendaji Mkuu wa chama ndiye katibu Mkuu aliyekiongoza chama katika kipindi cha upinzani mkubwa. Si siri kampeni za mwaka 2015 zilikuwa za kipekee ila kakivusha chama.
Anaelewana zaidi na vijana ndio maana katika kipindi chake cha Uongozi vijana wengi wamepewa nafasi na chama. Hata Umaarufu wa Nape uliongezeka chini ya Mbawa za Katibu mkuu Kinana (Ni mentor mzuri).
Ni mjenzi mzuri wa hoja kutokana na utulivu wake anavutia zaidi kumsikiliza. Hapendi siasa za kushambulia ni mtu anayesoma mchezo kabla ya kujibu hoja. Hakuna kiongozibwa upinzani anayetamani kukutana naye kwenye mdahalo hili lipo wazi kabisa.
Anapinga swala la waziri Mkuu kuwa mwenyekiti wa wabunge wa chama cha mapinduzi. Pia aliwahi kuwakemea wabunge wa Ccm KUKUBALI kila kitu Bungeni.
SIKU ZA KARIBUNI.
Siku za Karibuni Mh Kinana aliandika barua ya Kungatuka ila kutokana na Uzoefu wake Mwenyekiti wa Chama Mh Magufuli aliuomba mkutano mkuu kuridhia Kinana kuendelea na nafasi hiyo. Mkutano mkuu ulimpitisha kwa asilimia zote kuendelea na nafasi hiyo.
Siku za karibuni hajaonekana hadharani kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Mh Kinana alikuwa nje ya nchi ila kwa sasa amerejea kwa ajili ya mapambano.
Pia wadadisi wa mambo ya siasa wanadai kutokuonekana kwake kunatokana na kupewa mapumziko ya muda baada ya kazi kubwa aliyoifanya toka 2013 kuzunguka nchi nzima na kushiriki kampeni kwa asilimia kubwa.
Karibu Ofisini Tena Mh Kinana tutaanza kukuona mikoani, Vijiweni na kwenye media mbalimbali ukikijenga chama. Watanzania wapinzani kwa wana CCm wamekumiss kila Mtu anakuulizia.
Thadei Ole Mushi.