SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 4 Mei 2017

T media news

Kardinali Pengo aenda kutibiwa nchini Marekani

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesafiri kwenda Marekani siku ya Jumanne tarehe 2 Mei 2017 kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake pamoja na matibabu.

Kardinali Pengo anatarajiwa kuwepo huko nchini Marekani kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa ajili ya uchunguzi na matibabu yake..

Tuendelee kumuombea Baba Kardinali ili Mwenyezi Mungu amjalie nguvu na afya njema ya mwili na roho ili aweze kuliongoza vema Taifa la Mungu alilokabidhiwa.